Wed. Nov 5th, 2025
Wachezaji Joshua Mutale na Leonel Ateba Kutemwa Simba

Wachezaji wa Simba SC Joshua Mutale na Mshambuliaji Leonel Ateba wako Mbioni Kuondoka Simba baada ya Benchi la ufundi La Simba kutoridhishwa na Ubora wao.

Mutale amegomea matakwa ya Uongozi wa Simba wa Kumpeleka Singida Black Stars kwa Mkopo, Mutale amesema yupo Tayari Kuondoka Simba Endapo watakuwa Tayari kuvunja Mkataba na sio Vinginevyo.

Simba Wanafikiria Kumuuza Ateba kwenda katika Klabu ya Maghreb Fez ya Nchini Morocco ambayo imeonesha Nia ya kuhitaji Huduma ya Mshambuliaji huyo.

Lolote Linaweza kutokea kwa mmoja wa Wachezaji hawa kuelekea Msimu Ujao wa Mashindano.

ALSO READ | KUMEKUCHA: Yanga Wakana Kuichangia CCM Milioni 100, Wadai ni GSM