Wed. Nov 5th, 2025
Taifa Stars
Taifa Stars

CHAN 2024 | Shomari Salum Kapombe na Hussein Salum Masalanga ndio wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kwa upande wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambacho kinashiriki fainali za CHAN.

Wawili hao kwa sasa kila mmoja ana miaka 33, Kapombe amezaliwa Januari 28, 1992 wakati Masalanga yeye amezaliwa Machi 4, 1992.

Wachezaji wenye umri mdogo zaidi kwenye kikosi cha Stars ni Jammy Jammy ambaye amezaliwa Julai 15, 2006 na Wilson Nangu ambaye amezaliwa Julai 25, 2006.