Nyota wa PSG, Achraf Hakimi, anaripotiwa kukabiliwa na kesi ya ubakaji inayodaiwa kuwa aliifanya baada ya kumwalika mwanamke nyumbani kwake karibu na jijini la Paris. Waendesha mashtaka wa Ufaransa wametia saini hati ya mwisho ya mashtaka inayopendekeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 afikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya jinai.
Ijumaa, msemaji wa ofisi ya waendesha mashtaka wa Nanterre alithibitisha kuwa wameomba ‘jaji mpelelezi atoe uamuzi wa kupeleka kesi hiyo mahakamani. Hii inafuatia hatua ya Hakimi kushtakiwa rasmi kwa ubakaji Machi 03, 2023, na kuachiwa kwa dhamana akiwa chini ya uangalizi wa polisi
.
Iwapo atapatikana na hatia, raia huyo wa Morocco anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela ambayo ni adhabu ya juu kwa kosa la ubakaji huko Ufaransa
.
Kesi hii inahusiana na tukio la Februari 25, 2023. Kwa mujibu wa Le Parisien, mwanamke mwenye umri wa miaka 24 aliiambia polisi kuwa alikutana na Hakimi kupitia Instagram Januari mwaka huo. Baada ya mawasiliano ya mwezi mmoja, inadaiwa Hakimi alimtumia Uber kumleta nyumbani kwake huko Boulogne-Billancourt. Mke wake wa zamani mwenye asili ya Hispania na Uturuki, Hiba Abouk, 38, alikuwa likizo Dubai na watoto wao wawili wakati huo.
Mwanamke huyo anadai kuwa, alipowasili, Hakimi alianza kumbusu mdomoni na kwenye matiti kupitia nguo zake, licha ya kumkataza. Anasema kuwa baadaye alimfanyia unyanysaji bila ridhaa wa kijinsia yake na mwanamke huyo anadai aliweza kumsukuma Hakimi kwa kutumia mguu na akakimbia nje, kisha akamtumia rafiki yake ujumbe ili aende amchukue.
Alikwenda kituo cha polisi siku hiyo hiyo kutoa maelezo, ingawa awali alikataa kufungua rasmi kesi. Baadaye alitoa ujumbe alioutuma kwa rafiki unaoonyesha hali ya mshtuko aliyoipitia baada ya tukio hilo. Ilipofika Machi 03, 2023, Hakimi alishtakiwa rasmi na kuwekwa chini ya uangalizi wa mahakama lakini yeye mwenyewe amekuwa akikana tuhuma hizo hadi sasa
Disemba 8, 2023, mwanamke huyo alikabiliana uso kwa uso na Hakimi mbele ya jaji mpelelezi, ambapo aliweza kusisitiza tena madai yake, wakati Hakimi akikataa na kusema hana hatia yoyote. PSG ilimruhusu Hakimi kukosa mazoezi kwa kile walichokiita “sababu za binafsi”
