Wed. Nov 5th, 2025

“Lengo langu ni kufunga magoli mengi nikiwa hapa, nimechagua kuvaa jezi namba tisa

Najua Mayele ndiyo alikuwa akiivaa hii namba na tumewahi kucheza wote kwenye ligi moja Kongo yeye alikuwa As Vita mimi nilikuwa AC Rangers na baadae nikaenda FC Lupopo nilikuwa nikiongea nae hata alivyokuwa hapa Yanga

Alinieleza vitu vingi, ila aliniambia kuwa Yanga ndiyo klabu kubwa zaidi na Wana mashabiki Bora watakufanya ujisikie vizuri

Akaniambia kama nikipata ofa ya kwenda Yanga nisisite nije na nitafurahia maisha ya hapa na nitaweka kumbukumbu nzuri

Neno Moja kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba waendelee kujitokeza kwa wingi watimize upande wao kuipa nguvu timu na mimi nawaahidi nitafanya majukumu yangu vyema

Mashambuliaji mpya wa Yanga Andy Boyeli akizungumza kupitia Kipindi cha Transfer Talk cha Yanga TV.