Wed. Nov 5th, 2025
Kibu Denis
Kibu Denis

UPDATE: Nyota wa Simba Kibu Denis Kurejea Tanzania, Vipi Kuhusu Majibu ya Majaribio

Nyota wa Simba Kibu Denis (26) ataingia Tanzania jioni ya leo ili kuungana na timu kwenye pre-Season Misri.

Kibu anarejea nchini baada ya kumaliza majaribio yake nchini Marekani kwenye klabu ya Nashville SC.

Nashville SC Wamemwambia arejee Tanzania wakati wanachakata majibu yake ya majaribio,kama wataridhika na kiwango chake basi watatuma ofa ya kumnunua Simba.