Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino, ameipongeza rasmi Klabu ya Yanga kwa mafanikio yake makubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/25.
Katika salamu zake za pongezi, Infantino amesema kuwa ushindi huo si tu heshima kwa klabu hiyo, bali pia ni alama ya maendeleo ya soka barani Afrika, hususan kwa Tanzania.
“Napenda kuipongeza Yanga SC kwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/25. Mafanikio haya yanadhihirisha juhudi, nidhamu na mshikamano ndani ya timu na uongozi mzima wa klabu,” amesema Infantino.
