RASMI: Klabu ya Yanga SC imethibitisha kuachana na viungo Jonas Mkude na Clatous Chama baada ya muda mfupi tu tangu kujiunga nao wakitokea kwa watani wao wa jadi, Simba SC.
:
Hatua hii inafungua ukurasa mwingine katika historia ya usajili baina ya timu hizi mbili kongwe, ambapo wachezaji kadhaa waliowahi kung’ara wakiwa Simba wamehamia Yanga lakini baadaye kupoteza makali yao au kuachwa kabla ya muda wao kutimia.
:
Kwa sasa, huu ni mwendelezo wa mwenendo ambao unazua maswali mengi miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka: je, ni sajili za matakwa ya kocha au viongozi, au maamuzi ya kuona kama wanabomoa upande wa pili na badala yake mchezaji kama Okrah ilikazimika kwenda hadi FIFA kuidai klabu ya Yanga ?