Mangungu Sio Tatizo La Msingi

Mashabiki Maandazi wamekula viporo wameshiba hawana sehemu ya kuvipunguza zaidi ya kumnanga Mangungu eti ndio tatizo la Simba, Inawezekana kweli Mangungu ni sehemu ya tatizo lakini Simba kwa miaka kadhaa tatizo la msingi ni kuanzia mashabiki, wanachama na viongozi.Mashabiki maandazi wana uchungu kuliko wale wanaotoa pesa za mishahara ya wachezaji mbaya zaidi mashabiki maandazi hawajawahi kusema Mangungu sio Mwenyewe kiti wa klabu wakati Simba inacheza fainali ya shirikisho Caf hapa kuna dalili kubwa ya uvivu wa kufikiri.

Homa ya vipindi ya uwezo wa Joshou Mutale,kipaji mawe cha Ateba makosa ya kindezi ya Camara hapa mashabiki maandazi wanapiga kelele za Mangungu Mangungu ajiuzulu wanasahau Simba kuna mamilioni ya Mangungu wengine ambao labda wanahitaji zaidi lawama za kugongwa na Yanga.Mashabiki Maandazi wamesahau kabisa kuna Mangungu tatizo na wao ni tatizo kubwa kabisa.

Mashabiki Maandazi wanajiona kikundi cha waasi wakiamini kumpindua Mangungu ndio dawa ya kuacha kugongwa na mtani,hapa kuna zaidi ya kichekesho kwasababu Simba nzima imeshindwa kuuzima ubora wa Yanga.Simba angeweza kuwa bingwa mbele ya uso wa Mangungu lakini tatizo liko bayana kuhusu ubora wa Pacome na Joshou Mutale.

If truth shall kill them,Let them die 📌

@omarrkombo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *