Wed. Nov 5th, 2025

Huenda mshambuliaji wa Kitanzania na timu ya taifa “Taifa Stars’. Simon Msuva akasalia kwenye kikosi cha Al Talaba msimu ujao.

Kiwango bora alichoonyesha Msuva akiisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya nne kwenye mechi 38 za Ligi Kuu, ikishinda 18 sare tisa na kupoteza 11 kwa mabao yake 12 aliyofunga kimewashawishi viongozi wa timu hiyo kuendelea naye.

Nyota huyo wa zamani wa Wydad AC mkataba na klabu hiyo ulikuwa umeisha mwishoni mwa msimu huu na tayari timu imetoa ofa nono kwa Msuva.

Taarifa nilizozipata ni kuwa klabu imeshatoa ofa kilichobaki ni kwa mchezaji kama atakubaliana na dili hilo ama la. “Wiki iliyopita alisafiri kwenda Iraq kuna vitu vyake alikwenda kukamilisha ikiwemo hilo la kuongeza mkataba nafikiri huenda akabaki kwani wamemuwekea dili kubwa,” kilisema chanzo changu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *