Kumekucha..Wallace Karia Mgombea Pekee wa Urais TFF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, sasa amesalia kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa TFF katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 16, 2025, jijini Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Kamati ya Uchaguzi ya TFF, wagombea wengine waliokuwa wamechukua fomu hawakutimiza vigezo vilivyowekwa katika kanuni za uchaguzi, hali iliyomuwezesha Karia kupita katika mchujo wa awali bila kupingwa.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Wallace Karia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa TFF akiwa mgombea pekee, jambo linaloashiria ushawishi wake mkubwa ndani ya vyombo vya mpira wa miguu nchini. Uchaguzi huo utathibitisha rasmi uongozi wake kwa muhula mwingine iwapo hakutakuwa na pingamizi jipya litakalokubaliwa.