Garnacho aambiwa atafute timu ya kuchezea msimu ujao

Garnacho aambiwa atafute timu ya kuchezea msimu ujao

Meneja wa Manchester United, Ruben Amorim amewaambia wachezaji wa klabu hiyo kwamba ataendelea kusalia kuwa kocha wa klabu hiyo msimu ujao huku akiripotiwa kumwambia winga Alejandro Garnacho kutafuta klabu nyingine.

Hayo yametokea wakati wa kikao baina ya Mreno huyo na wachezaji katika uwanja wa mazoezi wa Man United wa Carrington huku kocha huyo akichukua uamuzi huo baada ya winga huyo kukosoa uamuzi wake kumchezesha winga huyo kwa dakika 20 tu kwenye fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur.

Awali iliripotiwa kuwa Garnacho (20) raia wa Argentina anathaminishwa na Euro milioni 70 ingawa dau hilo likitajwa kushuka wakati dirisha la usajili la kiangazi huku Napoli na Chelsea zikiwa miongoni mwa vilabu vinavyowania saini yake.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *