Simba mnawakosea mashabiki wenu✍️
Nimeona post ya Simba wakiwataarifu wanachama na mashabiki wao kuwa taarifa rasmi ya mechi ya pili itapigwa wapi itatolewa baada ya mechi ya mkondo wa kwanza.
Ukweli ni kwamba Barua ya CAF ilitumwa toka jana tarehe 14 kwenda TFF,na simba wamekuwa copied hivyo TFF na Simba wanajua ukweli kwamba mechi ya mkondo wa pili itapigwa Zanzibar Hakuna kingine✍️
Kwanini msiwambie ukweli mashabiki wenu mapema ili waache kununua ticket za Mkapa?
Mkiendelea kukaa kimya na watu 60 wakanunua ticket mtawaweka wapi wakati mnajua fika mechi itapigwa Zenji kwenye uwanja unaobeba watu 15,000?
Binafsi sitamani kuona machafuko na fujo ambazo mnaweze kuzikwepa kwa kuwambia ukweli wadau wa soka mapema
By Hans Rafael
ALSO READ | Baada ya Kelele Nyingi Kuhusu Uwanja Kuhamishwa Zanzibar, Simba Watoa Taarifa Hii