Wed. Nov 5th, 2025

Rais Samia Aipongeza Yanga Kwa Kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu 2024/25

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga Sc kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2024/25 kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba Sc katika dimba la Benjamin Mkapa.

“Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa 31 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ikiwa ni ubingwa wa nne mfululizo. Kwa zaidi ya miaka 85, upinzani wa Yanga na Simba umeendelea kuwa burudani kwa mamilioni ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Endeleeni kutupa burudani.”— ameandika Rais Samia kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *