Mchezaji Aziz K Hana Baya, Aitabiria Simba Kuchukua Ubingwa Mwaka Huu

Mchezaji Aziz K Hana Baya, Aitabiria Simba Kuchukua Ubingwa Mwaka Huu

Staa wa Yanga SC anayemaliza mkataba wake, Stephane Aziz Ki, ametoa kauli ya kushangaza lakini ya kiungwana baada ya kuisifia klabu hasimu ya Simba SC na kutabiri kuwa inaweza kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu huu.

Katika mahojiano na waandishi baada ya hafla ya jana usiku, Aziz Ki alionyesha heshima kwa wapinzani wao wa jadi, akisema kuwa Simba imeonesha kiwango kikubwa na cha kuvutia barani Afrika msimu huu.

“Ni wazi kabisa Simba wamekuwa bora sana kwenye michuano ya CAF msimu huu. Wanacheza kwa kujiamini, wanajua wanachokifanya na wameonyesha ukubwa wao. Kwa kiwango hiki, si jambo la kushangaza wakitwaa ubingwa,” alisema Ki kwa msisitizo.

Ki ambaye amekuwa akiongoza safu ya kiungo ya Yanga kwa kupachika mabao, alisema licha ya kuwa ni wapinzani wa jadi, mafanikio ya Simba katika anga za kimataifa ni fahari kwa soka la Tanzania kwa ujumla.

“Mwisho wa siku, wanabeba bendera ya taifa. Simba wakifanya vizuri, soka la Tanzania linaonekana. Kama watatwaa ubingwa, itakuwa historia kubwa kwa nchi,” aliongeza.

Kauli hiyo ya Aziz Ki imeibua mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii huku mashabiki wa pande zote mbili wakitoa maoni yao. Wengi wamepongeza ukomavu wa Ki, wakisema ameonyesha mfano mzuri wa jinsi wapinzani wanavyoweza kuheshimiana bila uhasama.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *