Rais wa Club ya Yanga SC, Injinia Hersi Said, ametajwa kama Kiongozi wa mfano katika mpira wa Afrika katika Jarida la African Leadership la Uingereza ambalo ni miongoni mwa Majarida makubwa duniani.
Jarida hilo huangazia Watu mashuhuri walio na mchango mkubwa katika nyanja mbalimbali kama siasa, uchumi, jamii, burudani na michezo.
Msemaji wa Club ya Yanga, Ally Kamwe ameeleza kuwa kutajwa huko kunatokana na mchango mkubwa wa Hersi katika maendeleo ya soka la Afrika ambapo tangu alipochukua uongozi wa Yanga SC mwaka 2022 amesimamia mageuzi makubwa ndani ya Club hiyo.
Mageuzi hayo ni pamoja na maboresho ya kiutawala, uimarishaji wa miundombinu na kuongeza hadhi ya Club kitaifa na kimataifa ambazo vilevile hatua hizo zimeendelea kuakisi mwelekeo mpya wa uongozi ndani ya soka la Afrika kwa ujumla.