Manara Yamkuta Makubwa, Afungiwa Ofisi za Manara TV na GSM Baada ya Kuvujisha Siri, Minyororo Yapigwa

Manara TV
Manara TV

Sakata la aliyekuwa msemaji maarufu wa klabu ya Yanga SC, Haji Manara, limechukua sura mpya baada ya taarifa kuibuka kuwa ofisi za Manara TV, zilizokuwa zikitumika katika ghorofa ya tano ya jengo la Salamander Tower, zimefungwa kwa minyororo kufuatia mvutano wa kimahusiano kati yake na Tajiri GSM, mmiliki wa jengo hilo.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na tukio hilo, inadaiwa kuwa Manara alikuwa akikaa bure kabisa katika ofisi hizo kwa muda mrefu bila kulipa kodi, gharama ya umeme, huduma ya WiFi, wala huduma nyinginezo, huku akifurahia ukarimu wa GSM aliyekuwa akimpa nafasi hiyo kama ndugu.

Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla baada ya madai kuibuka kuwa Manara alivujisha siri nzito zinazomhusu GSM, hali iliyosababisha uhusiano wao kuvurugika vibaya. Baada ya sakata hilo, Manara alipewa ‘notice’ rasmi ahame ofisini hapo, au, kama ana nia ya kuendelea kutumia ofisi hizo, basi alipie kodi ya mwaka mzima papo hapo.

Taarifa zinaeleza kuwa tangu atumiwe taarifa hiyo ya kuhama, Haji Manara hajafanya malipo yoyote wala kutoa majibu yoyote rasmi, jambo ambalo liliwafanya wamiliki wa jengo hilo kuchukua hatua kali ya kufunga kabisa ofisi hizo kwa makufuli na minyororo, huku baadhi ya vifaa vya Manara TV vikiwa bado ndani.

Tukio hilo limeibua hisia kali mitandaoni huku baadhi ya wafuasi wa Manara wakimpa pole kwa alichokutana nacho, na wengine wakisema ni “funzo kwa wale wanaochanganya urafiki na kazi bila maandalizi ya kisheria.”

ALSO READ: ORODHA ya Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking)

GSM, ambaye ni mwekezaji mkubwa wa Yanga SC na mfanyabiashara maarufu nchini, hajazungumza rasmi kuhusiana na tukio hilo, lakini wachambuzi wa masuala ya michezo na mitandao wanadai hili ni anguko la wazi kwa Manara TV, hasa kipindi hiki ambacho Manara alikuwa akijitahidi kujiimarisha upya baada ya kutoka Yanga SC.

Je, hili ni pigo kwa Manara au mwanzo wa ukurasa mpya? Mashabiki wake sasa wanasubiri kwa hamu kuona atajibu vipi kadhia hii.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *