Wed. Nov 5th, 2025

NAJARIBU KUWAZA KUHUSU UZOEFU!

Watu wa boli hivi naweza kuwa nafikiria vizuri kweli?

Ipo wazi Derby ina uzoefu wake. Kocha ambae ameshasimamia timu kwenye Derby kadhaa ni tofauti na kocha ambae hajawahi kabisa kuongoza timu kwenye Derby.

Mazingira ya Derby ya Kariakoo yana utamu na chungu yake. Hili linanipelekea kuwaza jambo moja muhimu sana

Fadlu Davids ameshaiongoza Simba kwenye Derby ya Kariakoo mara mbili, na mara zote alifungwa na Yanga

Hamdi Miloud anaingia kwenye hii derby ya leo akiwa hajui presha ya Derby ya Kariakoo, kwa ufupi Hamdi anaingia kama kuku mwenye kamba mguuni – Mgeni kabisa.

Kigezo cha uzoefu wa Derby hapa hakiwezi kweli kuamua matokeo ya hii mechi?

Au nyie watu wa boli mnasemaje?

Shaffih Dauda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *