Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Arsenal, Liverpool, Madrid zinamtaka Huijsen

Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Arsenal, Liverpool, Madrid zinamtaka Huijsen


Arsenal na Liverpool zinapambana kumsajili beki wa kati Mhispania kutoka Bournemouth, Dean Huijsen (20), ambaye pia anawindwa na Real Madrid. (Sky Germany)

Ingawa Huijsen anatamani kujiunga na Real Madrid, vilabu vya Ligi kuu England Liverpool, Arsenal na Chelsea, vipo tayari kutoa £50m kama mkataba wake wa sasa unavyotaka (Fabrizio Romano)

Manchester United wako mbele katika harakati za kumsajili mshambuliaji Mwingereza wa Ipswich Liam Delap, mwenye umri wa miaka 22, ambaye yuko tayari kujiunga na Old Trafford majira haya ya kiangazi (Sky Sports)

Nottingham Forest wanatarajia kusajili angalau wachezaji watano msimu huu wa joto, huku kiungo wa Manchester City James McAtee (22) na mshambuliaji wa Ipswich Liam Delap wakiwa miongoni mwa waliotazamwa (Telegraph)


Beki wa kulia wa Bayer Leverkusen kutoka Uholanzi, Jeremie Frimpong (24), anakaribia kutua Liverpool kwa uhamisho wa pauni milioni 29.5 (Mail)

Real Madrid wako karibu kutangaza usajili wa beki wa kulia Mwingereza Trent Alexander-Arnold (26) kutoka Liverpool, ingawa Liverpool wanadai fidia ya pauni 840,000 ili aruhusiwe kucheza Kombe la Dunia la Klabu. (ESPN)

Manchester United wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bournemouth kutoka Ghana, Antoine Semenyo (25), kuhusu kumsajili. (Talksport)

sChanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Antoine Semenyo
Brighton wako katika mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo mkongwe wa Kiingereza James Milner (29) (Athletic)

Winga wa Brazil Rodrygo (24) hataki tena kuchezea Real Madrid na anataka kuondoka klabuni hapo majira haya ya kiangazi (Marca)

Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Sporting Lisbon kutoka Sweden, Viktor Gyokeres (26), ambaye ana mkataba unaomruhusu kuondoka iwapo ada ya karibu pauni milioni 60 italipwa (Mirror)

Mbali na Gyokeres, Arsenal pia wana nia ya kumsaini mshambuliaji wa RB Leipzig kutoka Slovenia, Benjamin Sesko (21) (Sky Sports)

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *