WAKATI Ligi Kuu ikienda ukingoni. tayari rekodi ya ufungaji wa mabao msimu huu imevunjwa, tofauti na ilivyokuwa kwa msimu uliopita, ambapo hadi sasa yamefungwa jumla ya mabao 544, ikiwa ni idadi kubwa huku msimu ukiwa haujafikia tamati.
Katika mabao hayo 544 yaliyofungwa msimu huu, wachezaj wazawa wamefunga 292, wakigeni wakifunga 235 na ya kujifunga ni 17, huku msimu uliopita yakifungwa 517, ambapo nyota wazawa walifunga 299, wageni walifunga 206 huku ya kujifunga ni 12.