Wed. Nov 5th, 2025

Klabu ya Azam FC imefikia makubaliano ya kumuajiri Kocha Florent Ibenge kutoka DR Congo kuwa kocha mkuu wa timu hiyo. Baada ya makubaliano kukamilika, Ibenge ameondoka nchini na kwa sasa yupo Morocco akisubiri kuanza rasmi majukumu yake.

Taarifa zinaeleza kuwa Azam FC na Ibenge wamekamilisha masuala yote ya kifedha, na kocha huyo amekubali mradi wa klabu hiyo baada ya mazungumzo ya kina na uongozi pamoja na familia ya Bakhresa, wamiliki wa klabu hiyo.

Hata hivyo, miongoni mwa masharti ya Ibenge kabla ya kuanza kazi rasmi ni kutaka kiungo Feisal Salum “Fei Toto” asalie ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao, akiamini ni sehemu muhimu ya falsafa yake ya kiuchezaji.

Azam FC imepanga kuanza maandalizi ya msimu mpya mapema mwezi Julai, huku ikitarajia kuweka kambi barani Ulaya kwa ajili ya pre-season. Kocha Ibenge anatarajiwa kuungana na timu kabla ya safari hiyo kuanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *