Wed. Nov 5th, 2025

Mangungu Awaonya Wanaotaka Kuchukua Nafasi ya Karia Urais TFF

Mwenyekiti upande wa wanachama wa klabu ya Simba Sc mzee Murtaza Mangungu ni moja kati ya wadau wa kubwa wa soka nchini Tanzania ambao wameanza kufanya kampeni za chinichini katika kuhakikisha kwamba Rais wa sasa wa TFF Wallace John Karia anaendelea kusalia katika nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba siku chache zilizopita TFF walitangaza taarifa nzito kwa wadau wa soka juu ya uchaguzi mkuu wa nafasi ya Rais wa TFF pamoja na wajumbe 6 ambao watakuwa sehemu ya bodi ya viongozi wa TFF.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo ilikuwa imetolewa na TFF ni kwamba uchaguzi huo utafanyika mwezi Agosti uko jijini Tanga, mgombea yeyote ambaye anahitaji fomu ya kwenda kugombea nafasi ya Rais wa TFF anapaswa kwenda kuchkua fomu ambayo inatajwa kuwa na thamani ya pesa za kitanzania shilingi laki tano (500,000).

Katika kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba siku chache zilizopita mzee Murtaza Mangungu aliwai kutoa taarifa kwamba kwa mdau yeyote ambaye anahitaji kuja kugombea nafasi hiyo kwa sasa anapaswa kutoka hadharani na kuwaeleza watanzania kwamba atakuja kuleta maendeleo gani kwenye shirikisho hilo ambayo hayajafanywa na Rais Wallace Karia.

Mangungu anaamini kwamba hakuna mdau mwingine yeyote ambaye anaweza kuja kuwa Rais wa TFF na akaweza kufanya mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Wallace Karia hivyo anatamani kuona kwamba Rais huyo anaendelea kusalia madarakani licha ya kwamba baadhi ya watu wameanza kuonyesha nia ya kutaka kumuondoa kwenye nafasi hiyo.

Wallace Karia amefanya mambo makubwa sana kwa muda wote ambao amekuwa akihusumu kama Rais wa shirikisho hilo na pengine sasa anahitaji kupewa muda mwingine ili Tanzania iendelee kupiga hatua kwenye soka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *