Wed. Nov 5th, 2025

Pazia la michuano ya kombea Dunia kwa ngazi ya klabu limefunguliwa rasmi Alfajiri ya leo Juni 15, 2025 ambapo wawakilishi wa Afrika, Al Ahly ya Misri wametoshana nguvu kwa sare tasa na Lionel Messi na wenzake wa Inter Miami katika dimba la Hard Rock, Miami.

Wakati mashabiki wa Inter Miami wakitegemea maajabu kutoka kwa mshindi mara 8 wa Ballon d’Or, Lionel Messi, shujaa wa timu hiyo ya Marekani alikuwa kipa mkongwe Oscar Ustari (38) aliyeokoa hatari nyingi kutoka kwa Al Ahly ukiwemo mkwaju wa penalti wa Trezeguet muda mfupi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Hakuna timu iliyoona lango la mwenzake mpaka dakika ya 90 licha ya Inter Miami kuja kivingine kipindi cha pili na kupelekea kipa wa Al Ahly, Mohamed El Shenawy kufanya kazi ya ziada kwa kuzuia hatari kutoka kwa Tadeo Allende sambamba na nafasi mbili za hatari kutoka kwa Messi.

Al Ahly ipo Kundi A kwenye michuano hiyo sambamba na Inter Miami, Fc Porto ya Ureno na Palmeiras ya Brazil. FT: Inter Miami 🇺🇸 0-0 🇪🇬 Al Ahly

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *