Kocha Mkuu wa Simba SC Davids Fadlu ametoa kauli yake mara tu baada ya ushindi wao dhidi ya Simba SC. Simba SC ilipata ushindi wa 2-1 dhidi ya KMC FC jana. Kwanza, ameshukuru kikosi chake na kusema kuwa ushindi huo ni dhihirisho tosha ya mechi yao ya RS Berkane ya Morocco.
Mechi za viporo ambazo zilikuwa mezani kwa Kocha Fadlu Davids limefungwa rasmi jana Jumapili kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya Simba SC kukamilisha mechi nne kwa mafanikio makubwa kwa kukusanya pointi zote 12.
Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo huo wa nne mfululizo ndani ya siku 10. Simba ilikuwa na mechi nyingi mkononi kutokana na kushiriki kwao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, hali ambayo iliwafanya kuchelewa kucheza mechi kadhaa za ligi huku mpinzani wao, Yanga, ikiendelea na ratiba ya kawaida ya ligi.
Ushindi huo umeifanya timu hiyo kufikisha pointi 69 baada ya mechi 26, ikibaki nyuma kwa alama moja tu dhidi ya Yanga ambayo nayo imecheza idadi sawa ya mechi.
KMC ilikuwa ya kwanza kufungua pazia la mabao katika dakika ya nane kupitia kwa Rashid Chambo ambaye alifunga kwa shuti kali nje ya boksi likiwa ni bao la 11 Simba inaruhusu msimu huu.