Yanga SC walisimama imara dhidi ya Mamelodi Sundowns katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini wakapoteza kwa mikwaju ya penalti. Licha ya kushindwa kusonga mbele, lakini wachezaji kadhaa wa @yangasc walionyesha kiwango bora zaidi, wakivutia vilabu vya DStv Premiership.
Kwa mujibu FARPost, jukwaa la habari za michezo la mtandaoni la Afrika Kusini, wamewataja nyota watano wa Wananchi ambao wanaweza kuvivutia zaidi vilabu vya Afrika Kusini na pengine wakasajiliwa huko msimu ujao;
1. Djigui Diarra ๐ฒ๐ฑ (Golikipa)
2. Stephane Aziz Ki ๐ง๐ซ (Kiungo mshambuliaji)
3. Ibrahim Hamad ๐น๐ฟ (Beki wa Kati)
4. Maxi Nzengeli ๐จ๐ฉ (Kiungo mshambuliaji)
5. Yahya Mudathir ๐น๐ฟ (Kiungo)