Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Liverpool na Manchester United zinamuwania winga wa RB Leipzig Xavi Simons

 

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Liverpool na Manchester United zinamuwania winga wa RB Leipzig Xavi Simons

Mshambuliaji wa Uholanzi Xavi Simons huenda akaondoka RB Leipzig msimu huu wa joto na klabu hiyo ya Ujerumani italipisha takriban £70m endapo itaamua kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports Ujerumani)

Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa klabu ambazo zimekuwa zikimfuatilia Simons, ambaye mkataba wake na klabu ya RB Leipzig unaendelea hadi 2027. (Sport Bild – kwa Kijerumani)

Liverpool inakaribia kufanya mazungumzo ya kuamua mustakabali wa mshambuliaji wa Colombia Luiz Diaz, 28, mshambuliaji wa Ureno Diogo Jota, 28, na beki wa Ufaransa , 25, wakati ikielekea kwenye usajili la majira ya kiangazi. (Football Insider)

Waziri wa michezo wa Saudi Arabia Prince Abdulaziz bin Turki Al-Faisal anasema mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah “analingana na utambulisho wa kucheza” katika ligi kuu ya nchi hiyo lakini hakutaja kuhusu mazungumzo yoyote ya usajili baada ya mchezaji huyo wa miaka 32 kuongeza mkataba wake na Liverpool. (ESPN)

Mshambulizi wa Fiorentina Moise Kean ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 45 katika mkataba wake ambacho kinaweza kutumika kuanzia Julai 1-15. Licha ya kuhusishwa na vilabu kadhaa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kusalia na Viola ili kuimarisha nafasi yake ya kujumuishwa katika kikosi cha Italia cha Kombe la Dunia la 2026. (Tuttomercatoweb – kwa Kiitaliano)

Everton itamruhusu mlinzi wa kati wa Uingereza Michael Keane, 32, kuondoka katika klabu hiyo mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa mweizi Juni. (Football Insider)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco amedokeza kwa kipa wa Poland Wojciech Szczesny, 35, atasaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kusalia katika klabu hiyo ya Catalan. (Marca kwa Kihispania)

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *