Yanga SC wamefuzu fainali ya Kombe la Muungano, Kipa Mshery Aibuka Kuwa Shujaa

Mshery

Dakika za mwisho Mshery amekua shujaaa wa mchezo akidaka penalti 2 huku moja Zimamoto wakigongesha mwamba…Na mikono yake imewapeleka Wananchi Fainali…Imekua mikwaju yenye thamani kwa Mshery.

Yanga SC wamefuzu fainali ya Kombe la Muungano lakini kwa presha kubwa..Dakika nyingi walishikilia roho mkononi

Licha ya Zimamoto kutolewa lakini wameonyesha kiwango bora na sanaa ya kucheza kwa hari ya upambanaji na kujituma.

Nimeshuhudia kiwango bora kutoka kwa Zimamoto mbele ya Yanga SC “Timu yenye quality kubwa”.


Yanga SC watakutana na JKU katika fainali ya Kombe la Muungano baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 3-1 mbele ya Zimamoto

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *