USHINDI wa mabao 2-1, ilioupata Simba dhidi ya Mashujaa FC, kwenye Uwanja wa KMC Complex Mwenge, Mei 2, 2025, umekifanya kikosi hicho cha Msimbazi kufikisha jumla ya mechi 17, mfululizo za Ligi Kuu bila ya kupoteza.
Mara ya mwisho kwa Simba kupoteza, ilikuwa ni kichapo cha bao 1-0, dhidi ya Yanga, Oktoba 19, 2024, hivyo kuanzia hapo imecheza mechi 17, mfululizo bila ya kuonja ladha ya kichapo, ambapo kati ya hiyo imeshinda 15 na kutoka sare miwili.