Jose Luis Riveiro Atajwa KOCHA Mpya Yanga

Jose Luis Riveiro Atajwa KOCHA Mpya Yanga

YOUNG AFRICANS ina mpango wa kuwa na benchi jipya la ufundi kwa msimu ujao, taarifa zinadai kuwa mabosi wa timu hiyo wametua Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kocha Jose Luis Riveiro ambaye kwa sasa anaifundisha Orlando Pirates ya nchini humo.

Kocha Jose huu ni msimu wake wa mwisho ndani ya Orlando Pirates kwani tayari amewaambia mabosi wa timu hiyo hataongeza mkataba utakapofikia tamati Juni 30, mwaka huu. Taarifa za ndani ya Yanga zinasema kuwa kuna mazungumzo yanafanyika kati ya uongozi wa timu hiyo na kocha na Kocha Jose wa Orlando Pirates ili aje kuwa kocha mkuu kwa msimu ujao.

“Kilichotuvutia zaidi ni rekodi zake ikiwemo msimu huu kuifikisha Orlando Pirates nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, lakini hata kwa upande wa ligi ya ndani anafanya vizuri,” kilisema chanzo changu makini ndani ya Yanga.

Mbali na Yanga, pia kocha huyo ana ofa ya Saudi Arabia, huku pia akihusishwa na Al Ahly ambayo hivi karibuni iliachana na kocha Marcel Koller baada ya kushindwa kuifikisha timu hiyo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Jose tangu ametua Orlando Pirates Julai 1, 2022, amefanikiwa kushinda mataji matatu ya Kombe la MTN na mawili ya Kombe la Nedbank huku msimu huu timu hiyo ikiishia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikipoteza mbele ya Pyramids.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *